Saturday, 31 October 2015

HAYA NI MAMBO HATARI UNAYOPASWA KUYAJUA MWANAMKE YANAYOWEZA KUSABABISHA MIMBA ZAKO KUTOKA MARA KWA MARA

Habari za weekend mdau wangu wa www.dkmandai.com bila shaka umzima wa afya tele na unaendelea na shughuli zako vizuri kabisa.

Leo nimeona ni vyema tugusie hili suala la kuharibika kwa mimba mara kwa mara angalau tuzifahamu hata sababu zake tu.

Naamini kwamba kila mwanamke anapobeba mimba matarajio yake huwa ni kujifungua salama na baadaye kumfurahia mtoto wake, licha ya kwamba baadhi ya wanawake kwao imekuwa ni ngumu kuifikia hiyo furaha ya kupata mtoto kwani baadhi yao huishia kubeba mimba tu kisha baada ya mda utasikia imetoka!

Leo wacha tuzifahamu sababu ambazo huchangia tatizo hili la kuharibika kwa mimba mara kwa mara kama ifuatavyo>>>

Moja ya sababu ni maambukizi kwenye mji wa uzazi wa mwanamke kuna kitu huitwa Pelvic Inflammatory Diseases (PID) yaani kuvimba kwa kuta za mji wa mimba au kuvimba kwa mirija ya uzazi.

Sababu nyingine ambayo huweza kuchangia kuharibika kwa mimba mara kwa mara ni matatizo ya fangasi Candida nazo pia kwa nafasi yake huchangia sana tatizo hili.

Historia ya utoaji wa mimba mara kwa mara huweza kuwa sababu ya tatizo hili, wanawakie au wasichana wenye tabia ya kutoa mimba moja au mbili au tatu basi nao huweza kuwa katika hatari ya kuingia katika tatizo hili baadaye.

Chanzo kingine kikubwa ni magonjwa ya zinaa {sexually transmitted diseases}, magonjwa kama kaswende, kisonono,mara nyingi sana huathiri mfumo wa uzazi wa mwanamke na hasa hasa kwenye mji wa mimba na kuufanya kuwa legevu na hata ujauzito unapotunga basi huweza kutoka kirahisi.

Kwa maelezo zaidi au kama unatatizo hilo au kama rafiki au ndugu yako anatatizo hilo usisite kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment