Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 15 October 2015

HII NDIO LIST YA MATUNDA YENYE UWEZO WA KUFANYA NGOZI YAKO KUWA VIZURI ZAIDI


Ngozi ni moja ya sehemu muhimu sana kwa mwili wa binadamu na ndiyo imefunika sehemu kubwa ya miili yetu.

Ulaji wa vyakula ni mojawapo ya mambo muhimu ambayo huweza kumfanya mtu kuwa na ngozi nzuri yenye kupendeza zaidi.

Vifuatavyo ni miongoni mwa vyakula muhimu kwa afya ya ngozi

Machungwa.
Machungwa ni mojawapo ya tunda ambao hufaa sana kwa afya ya ngozi zetu, hii ni kwa sababu tunda hili lina vitamin C yakutosha ndani yake ambayo husaidia sana uundaji wa seli mpya za ngozi, lakini pia ulaji wa tunda hili husaidi sana kuboresha rangi ya ngozi zaidi.

Maparachichi
Tunda hili moja ya sifa yake ni kuwa nauwezo mzuri wa kuirutubisha ngozi na kuipatia unyevunyevu hasa kwa wale wenye ngozi kavu.

Parachichi pia limesheheni virutubisho ikiwa ni pamoja na vitamin C, E, K pamoja na folic acid, magnesium na potassium vyote kwa pamoja ni muhimu sana kwa siha ya ngozi.

Tunapozungumzia kuhusu vitamin E yenyewe hufanya kazi kubwa ya kuulinda ngozi dhidi ya mikunjo na uharibifu unaotokana na miale ya jua pamoja na athari za moshi wa sigaraKwahiyo kutokana na hayo unashauriwa kutumia tunda hili mara kwa mara ili kuwa na afya bora zaidi, lakini pia unaweza kuchanganya maziwa kidogo na parachichi kisha ukatumia mchanganyiko huo kwa kupaka usoni na utakaa nao kwa dakika kumi ili kupata matokeo mazuri zaidi

Nyanya.
Nyanya nayo haiukusaulika kwani inauwezo mzuri wa kumfanya mhusika kuendelea kuonekana mwenye ngozi nzuri hata kama umri utakuwa umeenda.

Hivyo unaweza kujitahidi kutumia nyanya mara kwa mara, na ukiweza pata mchanganyiko wake na uwe unapaka usoni kisha acha kwa dakika 10 kabla ya kuosha fanya zoezi hilo kila siku kwa matokeo mazuri zaidi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment