Saturday, 3 October 2015

HIVI NDIVYO MWANAMKE ANAVYOWEZA KUSABABISHA MWANAUME KUKOSA NGUVU ZA KIUME

Mara kadhaa tumeshazungumza kuhusu tatizo la nguvu za kiume, lakini pia tumeshazungumza sana kuhusu sababu za tatizo hili, dalili na hata namna ya kukabiliana nalo.

Hata hivyo, mara nyingi tumekuwa tukieleza sababu za tatizo hili za nguvu za kiume ambalo huchangiwa na tabia za wanaume wenyewe, lakini leo nataka tuangalie namna mwanamke anavyoweza kumsababishia mwanaume kuingia kwenye janga hili la upungufu wa nguvu za kiume

Miongoni mwa sababu ambazo huweza kusababishwa na mwanamke na kupelekea mwanaume kuingia kwenye janga la tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na hizi zifuatazo:-

Kutokuwepo kwa mazingira ya usafi kwa mwanamke:
Hali ya usafi ni muhimu hasa zile sehemu muhimu ambazo huusika kwenye tendo la ndoa endapo mwanamke atakuwa si msafi basi huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Naamini kwamba kila mtu hupenda usafi na wengi wetu tunafahamu kero za uchafu wakati wa teno, kwa mantiki hiyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa.

Mwanamke kuwa msafi ni muhimu sana, kuanzia mavazi na mwili pia hii itasaidia kuleta msisimko zaidi katika mapenzi.

Kutokuwa na uhodari na ujuzi
Wanawake wengi huhofia sana kuonesha ujuzi wao wa kimapenzi wanapokuwa na wapenzi wao, huku wengi wakiogopa kuhisiwa huenda ni wazoefu zaidi katikamasuala hayo, lakini si kweli ujuzi na uhidari kwa mwanamke ni muhimu zaidi kwani huleta hamasa kwa mwanaume na hivyo kumsaidia kuepukana na shida ya upungufu wa nguvu za kiume.

Tatizo hili lipo zaidi kwa wanawake ambao tayari wapo ndani ya ndoa, wengi wao huwa hawajishughulishi kumsaidia mwanaume kupata mihemko zaidi na wala hawana ubunifu jambo ambalo humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea hisia zake mwenyewe pekee, hali ambayo si nzuri kwani mwanaume ikitokea atakuwa na mawzo au kuchoka hatoweza kupata mhemko kwasababu hapati ushirikiano toka kwa mwenzake (mwamke).

Maneno ya karaha
Pale inapotokea mwanamke akawa ni mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi basi hali hiyo huweza kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Jambo ambalo baadaye husababisha wanaume wengi kuanza kutoka nje ya ndoa zao.

Hayo ni machache kuhusu sababu ambazo mwanamke huweza kumsababishia mwanaume tatizo la nguvu za kiume, lakini kama unahitaji ushauri zaidi kuhusu tatizo hili unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0769 400 800, 0784 300 300, 0716 300 200.

No comments:

Post a Comment