Monday, 12 October 2015

HIVI NDIVYO VYAKULA VYENYE UWEZO WA KULINDA AFYA YA INI LAKO


Ini ni moja ya kiungo muhimu sana katika mwili wa mwanadamu. na ni mojawapo ya kiungo ambacho kinahitaji kulindwa vizuri kutokana na umuhimu wake mwilini.

Ini lina kazi ya kuchuja sumu mwilini ambapo huchuja sumu kwenye damu ambayo huingia kwa njia ya vyakula na vinywaji (bila kusahau vinywaji vikali), hewa tunayovuta, sigara, pamoja na dawa tunazotumia kila siku.

Pia ini hutoa nyongo ambayo kazi yake kubwa ni kusaga mafuta na protini kutoka kwenye chakula tulacho, lakini pia, ini hukibadilisha chakula na kufanya tupate nguvu mwilini.

Hivyo basi, tunahitaji kulilinda ini ili liweze kufanya kazi yake ya uondaji wa sumu na kusaga mafuta na protini kama ilivyokusudiwa.

Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula ambavyo vitasaidia kulinda afya ya ini lako>>>>>>
Kitunguu saumu: 
Inasaidia ini kutoa viashiria ambavyo husaidia kuondoa sumu kwenye mwili, pia husaidia kulilinda ini lisiharibiwe na sumu.

Pia kitunguu saumu husaidia kupunguza cholesterol mwilini ambapo inapozidi sana hulipatia kazi kubwa ini ya kuchuja sumu.

Unaweza kutafuna punje 2 au 3 kila siku za kitunguu saumu au kuweka kwenye chakula chako ili kuisaida ini yako zaidi.

Parachichi
Tunda hili nalo linasifika sana kwa kuwa na uwezo wa kusafisha ini na kulilinda ini ili lisiharibiwe na sumu.

Limao
Limao husaidia sana pia kusafisha ini na kuifanya utendaji kazi wake kuwa mzuri zaidi

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe ni dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment