Thursday, 22 October 2015

HIZI NDIO SABABU ZINAZOCHANGIA KUTOKWA NA JASHO JINGI MWILINI

Habari za leo mpendwa msomaji wangu wa www.dkmandai.com leo napenda tuzungumze kuhusu tatizo la kutokwa na jasho kupita kiasi.
Nimeamua kuzungumzia hili leo kutokana na kupokea maswali mengi ya watu wakihitaji kufahamu zaidi kuhusu tatizo hili.
Kwanza ni vizuri ikafahamika kwamba kutokwa jasho ni njia mojawapo ya mwili kutoa taka, lakini pia  ni mfumo unaotumiwa na mwili ili kuupooza pale hali ya hewa au joto la mwili linapokuwa limepanda.
Kila mtu huweza kutokwa na jasho, lakini kwa kawaida mwili hutoa jasho baada ya mtu kufanya shughuli fulani ya kufanya joto la mwili kupanda, lakini pia jasho huweza kutoka endapo mhusika atakumbwa na msisimko fulani, basi hapo  pia jasho linaweza kumtoka.
Aidha kuna baadhi ya watu ambao mbali na sababu hizo hapo juu, huweza kujikuta wakitokwa na jsho licha ya kuwa hawajafanya shughuli yoyote wala hawajakumbwa na msisimko wa aina yoyote ile na kitaalam tatizo hilo hufahamika kama 'hyperhidrosis.'

Kwa ujumla kuna baadhi ya matatizo ya kiafya ambayo huchangia tatizo hili la kutokwa na jasho ikiwa ni pamoja na matatizo ya neva zinazohusiana na glandi za jasho katika mwili na kuzifanya glandi zifanye kazi zaidi ya inavyohitajika, pia tatizo hili huhusishwa na kurithi.

Sababu nyingine ni matumizi ya baadhi ya dawa, mfano dawa za kuondoa msongo wa mawazo, dawa za kutibu matatizo ya saratani, halikadharika na dawa zinazotumika kutibu matatizo ya uzazi.

Pia kuna baadhi ya magonjwa ambayo huweza kusababisha mtu apate tatizo hili, mfano kifua kikuu na dalili za homa pia.
Pamoja na hayo wanawake ambao hufikia hatua ya kukoma kwa hedhi menopause nao baadhi yao huweza kuwa na tatizo hili japo si wote na si lazima imkute kila mmoja anapofikia hatua hiyo

Hayo ndiyo machache ambayo nimeona nikujuze kuhusu tatizo hilo, lakini kama unatatizo hilo na unahitaji msaada basi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment