Tuesday, 20 October 2015

HIZI NDIO SABABU ZINAZOPELEKEA BAADHI YA WANAWAKE KUKOSA HEDHI

Add caption
Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo. 

Pia tatizo hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbwa na tatizo hilo.

Kitaalam tatizo la kukosa hedhi huitwa 'amenorrhea' na visababishi vya tatizo hili ni pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni: Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa chanzo cha tatizo hili.

Lishe duni nayo ni miongoni mwa sababu ya tatizo hilo, hivyo mwanamke anayekosa lishe bora huweza kujikuta akiingia katika tatizo hili bila kutarajia, hivyo ni vyema kuzingatia ulaji wa lishe bora.

Mtumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango huweza kuchangia tatizo hili kwa baadhi ya wanawake licha ya kwamba si wanawake wote huweza kupatwa na hili tatizo kutokana na sababu hii.

Sababu nyingine za tatizo hili ni pamoja na msongo wa mawazo, matumizi holela ya dawa, kuishi kwa hofu iliyopitiliza ufanyaji wa mazoezi kupita kiasi pamoja na uwepo wa magonjwa sugu kwa mhusika.

Ni vyema ikafahamika kuwa tatizo hili si ugonjwa bali ni dalili za kuwepo kwa tatizo, lakini pia tatizo hili huweza kusababisha mwanamke kushindwa kushika mimba ikiwa tatizo hilo halitashughulikiwa mara moja.

Kama unasumbuliwa na tatizo hili ni vyema ukawasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment