Wednesday, 21 October 2015

HUU NDIO UMUHIMU WA JUISI YA MACHUNGWA KWA AFYA YAKO, NI KINGA DHIDI YA SARATANIKwa kawaida tumezoea kutengeneza juisi za aina mbalimbali katika familia zetu na si wote huwa tunatambua umuhimu wa juisi hizo kiafya, lakini badala yake wengi huwa tunafurahishwa tu na ladha nzuri zitokanazo na vimiminika hivyo vitokanavyo na matunda.

Leo napenda tuzungumzie faida za matumizi ya juisi ya machungwa kwa afya zetu.

Kimsingi chungwa ni mojawapo ya tunda lililosheheni uwingi wa virutubisho vingi ikiwa ni pamoja na vitamin C, A, pamoja na madini ya 'potassium', 'magnesium', 'copper', 'folate,' 'flavonoids'  pamoja na protini ya kutosha pia.

Kwanza kabisa juisi ya chungwa ina sifa ya kuimarisha kinga za mwili na kuzifanya kuwa imara zaidi, hii ni kwa sababu uwepo wa vitamini C huamasisha kinga za mwili kuwa katika ubora zaidi.

Juisi ya chungwa ni kinga dhidi ya saratani, hii ni kwa sababu juisi ya chungwa inakirutubisho kiitwacho 'antioxidants' ambayo ni nzuri kwa kinga ya saratani.

Lakini pia 'antioxidants' si kinga tu ya saratani lakini pia husaidia sana kuthibiti magonjwa mbalimbali hususani yale sugu.

Kazi nyingine muhimu ya juisi hii ya chungwa ni kurahisiha mzunguko wa damu mwilini, ndani ya chungwa kina kitu kiitwacho folate, ambayo huchangia uwepo wa vitamin B9 ambayo ni muhimu sana kwa kutengeneza vinasaba vya mwili pamoja na uundaji wa seli mpya ndani ya mwili.

Kwa ushauri na amaelezo zaidi tunapenda kukukaribisha sana Mandai Herbalist Clinic au tupigie simu sasa kwa namba za simu zifuatazo 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment