Saturday, 17 October 2015

IFAHAMU HII MITI YA AINA 3 YENYE UWEZO MZURI WA KUWASAIDIA WALE WENYE TATIZO LA KISUKARI


Kisukari ni ugonjwa unaotokana na matatizo ya mfumo wa uyeyushwaji wa chakula ndani ya mwili.

Ukosefu au upungufu wa kemikali inayoitwa insulin husababisha ongezeko la sukari inayojionesha kwa kiwango kikubwa katika haja ndogo ya muathirika pia.


Miongoni mwa sababu ambazo hupelekea ugonjwa huu ni pamoja na kuishi maisha ya anasa, watu wasiojishughulisha na kazi za kutumia nguvu au mazoezi na wale wanaopenda kutumia vyakula vilivyotengenezwa kwa kuongezwa sukari.


Dalili za mtu mwenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja na kukojoa mara kwa mara, kuhisi njaa mara kwa mara, kuhisi kiu ya maji mara kwa mara, kupungua uzito wa mwili pamoja na kuchoka kwa mwili mara kwa mara.


Hata hivyo ni veyama ikatambulika kuwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari hayalengi katika kuponya ugonjwa , ila ni kumsaidia mgonjwa aweze kuishi maisha ya kawaida na miongoni mwa tiba asili inayoweza kumsaidia mgonjwa wa kisukari kuishi maisha ya kawaida ni pamoja na matumizi ya majani ya mlonge na mwembe.

Tbibu Abdallaha Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anabainisha kuwa majani ya mwembe yanapokuwa machanga na kulowekwa ndani ya maji safi na salama kisha kukamua maji hayo na kunywa glasi ya maji hayo humsaidia sana mgonjwa wa kisukari kurekebisha sukari yake ndani ya mwili.
Mti wa muembe
Lakini pia majani hayo ya mwembe yanaweza kukaushwa kupitia kivuli kisha baada ya kukauka vizuri saga yawe unga laini na utumie kijiko cha chai katika glasi ya maji mara tatu kwa siku.
Mti wa zambarau

Pia zambarau huweza kumsaidia mgonjwa wa kisukari hii ni mara baada ya kuzikausha na kuzisaga ili kupata unga laini, kisha tumia nusu kijiko cha chai cha unga wa zambarau katika glasi ya maji kila siku asubuhi kabla ya kula chochote.

Mbali na hayo, Tabibu Mandaia anaeleza kwamba majani ya mlonge nayo ni moja ya msaada mzuri kwa wenye kisukari kwani husaidia kurekebisha sukari ndani ya mwili, hii ni kutokana na uwezo wa majani hayo kuwa na uwezo mzuri wa kurekebisha kongosho na kuifanya ifanye kazi yake vyema mwilini.

Kuhusu maelezo zaidi juu ya kuandaa haya majani ya mlonge ili yaweze kukusaidia ni vyema ukamsikiliza mwenyewe hapa chini Tabibu  Mandai akielezea. Karibu sana>>>
Pamoja na tiba zote zilizoorodheshwa hapo juu mazoezi ya viungo ni muhimu kila siku, mazoezi hayo ni pamoja na kutembea na kukimbia na mazoezi ya viungo pia ni vyema ukazingatia kutumia mboga za majani.


Kwa ushauri zaidi fika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana na Tbibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

8 comments:

 1. I wanted to thank you for this excellent read !! I loved every little bit of it. I have you bookmarked your site to check out the new stuff you post.
  Valentines Day Images Free Download

  ReplyDelete
 2. Post very nicely written, and it contains useful facts. I am happy to find your distinguished way of writing the post.
  Valentines Day 2018 Images
  Happy Valentines Day 2018 Images
  Valentines Day 2018 Images

  ReplyDelete