Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 16 October 2015

IMETHIBITIKA MBUNGE DEO FILIKUNJOMBE AMEFARIKI RIP

Ni dhahiri kwamba kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii basi utakuwa ulisikia ripoti za kuhusu ajali ya Helikopta iliyotokea jioni ya Oktoba 15, 2015 katika Hifadhi ya Wanyama ya Selous, pembeni mwa Mto Ruaha.

Katika taarifa zilizokuwa hazijathibitishwa bado ilikuwa ni kuhusu kufariki kwa Mhe. Deo Filikunjimbe ambaye alikuwamo kwenye helikopta hiyo iliyopata ajali.

Sasa Jerry Silaa amepost Ujumbe huu akithibitisha kufariki kwa Mbunge Deo Filikunjombepamoja na baba yake, Mzee William Silaa ambaye alikuwa Rubani wa Helikopta hiyo .“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajiali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha…. Nimepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William Silaa, nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe.Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani“ hayo ni maneno yaliyoandikwa na Jerry Slaa
Marehemu Deo Filikunjombe
“Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi. Namshukuru Mhe.Rais Jakaya M Kikwete, Dr.John Pombe Magufuli, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu MU Dr.Meru, Kampuni ya Everest Aviation ,Wabunge, MaDC, Maafisa wa TCAA na wote walioshiriki kuwatafuta wahanga wa tukio hili. Tutajuzana taarifa na mipango mingine. JS” Jerry Slaa

No comments:

Post a Comment