Tuesday, 27 October 2015

JE, KUNA MADHARA KUJAMIANA WAKATI MWANAMKE AKIWA KWENYE SIKU ZAKE (HEDHI)? MAJIBU YAPO HAPA

Habari za leo mdau wa www.dkmandai.com naamini mambo yanaendelea vizuri popote pale ulipo na amani itakuwa imetawala, huku ukiendelea kupokea matokeo mbalimbali ya uchaguzi kupitia vyombo vya habari.

Sasa wakati ukiendelea kupokea matokeo hayo ni vyema kwa sasa nijibu mojawapo ya swali lililoulizwa na mdau wa tovuti hii ambaye yeye aliomba kujua endapo akijamiania na mwanamke ambaye yupo hedhini kama kuna madhara yoyote.

Nitaanza kulijibu swali hilo kama ifuatavyo kwamba kujamiana na mwanamke akiwa katika hedhi hakuna madhara yoyote yaliyothibitishwa kiafya kutokea kutokana isipokuwa kitendo hicho huweza kuwasababishia wahusika kuweza kupatwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kirahisi zaidi ikiwemo gonjwa la  UKIMWI.

Lakini mbali na sababu hiyo pia jambo hili si nzuri kwani huweza kumsababishi mwanamke maumivu zaidi na kushindwa kufurahia tendo hilo na hivyo hali hiyo huweza kupelekea mwanamke kuchukia kabisa tendo la kujamiana.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment