Friday, 23 October 2015

JE, UNAFAHAMU KUWA KUKAA NA MKOJO KWA MUDA MREFU KUNA MADHARA? SOMA HAPA UELEWE KUHUSU HILI


Kuna wakati huenda huwa unajikuta umebanwa na haja ndogo (mkojo) na upo kwenye mazingira magumu ya kuweza kumaliza haja yako hiyo.


Inawezekana ukakubwa na hali hiyo ukiwa kwenye mkutano muhimu sana au safarini na bado haijafika zile sehemu zetu za kupata haja maarufu kama 'kuchimba dawa' na hivyo ukajikuta ukishindwa kabisa kutoa haja hiyo na kuendelea kujibana na kuvumilia hali hiyo kwa kipindi kirefu.

Lakini huenda baadhi yetu hatufahamu kuwa huwa kuna madhara ya kukaa na mkojo kwa muda mrefu bila kuutoa, hivi ni mara ngapi umesikia mtu akisema "mkojo umenibana sana, lakini ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia" ni wazi kwamba wengi wetu huwa tunasema hivyo mara kadhaa.

Kw kawaida kutokana na vinywaji tunavyokunywa husababisha mkojo kujaa kwenye kibofu cha mkojo na hapo ndipo mtu huanza kuhisi hitaji la kwenda kukojoa na ifahamike kwamba kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi asili vinavyopeleka taarifa kwenye ubongo kuonyesha kuwa kibofu cha mkojo kimekaribia kujaa au tayari kimejaa, baada ya taarifa hizi kufika katika ubongo, ubongo unatoa taarifa katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia mkojo huo kwa kuikaza misuli maalumu mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa utakapofika.

Sasa pale inapotokea mhusika aliyebanwa na mkojo akapuuza kwenda kukojoa hali husababisha ubongo kuendelea kupata usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha mkojo na kwa kuwa ubongo nao hutuma taarifa katika kibofu cha mkojo kusema kuwa mkojo uendelee kushikiliwa mpaka muda muafaka utakapofika, 

Lakini hali hiyo ya kutokojoa kwa wakati inapoendelea hufika wakati uwezo wa ubongo kutoa taarifa hizi na pia uwezo wa vigunduzi asili vilivyoko katika kibofu cha mkojo hupoteza uwezo wake tena wa kufanya kazi hizo au kuwa na uwezo mdogo, jambo ambalo husababisha tatizo kwa mhusika kuwa na uwezo mdogo wa stahimili kukaa na mkojo na hivyo itakuwa muda mdogo tu….mtu tayari kaloanisha nguo yake.
Pia kujibana huko hupelekea misuli maalumu ya kubana mkojo (sphincter) kushindwa kuvumilia kwa muda mrefu, lakini pia endapo mkojo utashindwa kutoka kwa wakati huweza kutengeneza mazalia ya bakteria na kukusababishia magonjwa ya kibofu (bladder infection). ikiwa ni pamoja na U.T.I (Urinary Tract Infections), sambamba na magonjwa ya figo na mchafuko wa damu.

Baada ya kufahamu madhara hayo ya kukaa na mkojo kwa muda mrefu sasa ni vyema tukaanza kuwa wasikivu pale tunapobanwa na mkojo, hii ni kwa ajili ya afya ya kibofu chako cha mkojo lakini pia ni kwa ajili ya afya yako kwa ujumla.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment