Wednesday, 28 October 2015

JE, UNASUMBULIWA NA TATIZO LA HARUFU MBAYA YA MIGUU? SOMA HAPA


Ishu ya miguu kutoa harufu mbaya ni tatizo sugu linalowakabili baadhi ya watu katika jamii, wengi wao wakiwa ni wanaume. 

Licha ya kuwepo kwa sababu mbalimbali zinazochangia kutokea hali hiyo, ukweli ni kwamba tatizo hili kwa kiasi kikubwa huchangia na uchafu.

Pamoja na kuwepo kwa tiba mbalimbali za kitaalamu ambazo mtu mwenye tatizo hili anaweza kupata, usafi ni jambo la msingi na kuzingatiwa ili kukabiliana na tatizo hili.

Hivyo ikiwa utagundua kuwa una tatizo hili, hakikisha unasafisha miguu, viatu na soksi zako mara kwa mara ili kuepusha unyevunyevu.

Pia ili kukabiliana na tatizo hilo ni vizuri kuepuka kurudia soksi au kuvaa ambazo hazijakauka vyema kwani zinaweza kusababisha miguu kunuka mara dufu, lakini pia epuka kuvaa viatu vilivyoloa na endapo ikatokea umenyeshewa, hakikisha unavianika kwenye hewa ili vikauke kupunguza uwezekano wa kutokea harufu.

Unaweza kusugua miguu kwa kutumia chumvi na kuvaa open shoes ili kuepuka tatizo ili.Ikishindikana, ni vyema kuonana na wataalamu wa afya. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi  kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmailcom 

No comments:

Post a Comment