Monday, 12 October 2015

JITIBU MAJERAHA YAKO KWA VITU ASILIA IPO PIA ALOE VERA, SOMA HAPA UJUE NA VINGINE ZAIDI


Habari za leo mdau wa www.dkmandai.com bila sha umzima wa afya ikiwa leo ni Jumatatu ya Octoba 12, 2015 ni vizuri tuendelee kujuzana mambo mengine muhiu kuhusu afya zetu kwa ujumla.

Moja ya mambo ambayo napenda kuzungumzia kwa sasa ni kukufahamisha mambo ya kufanya pale unapopatwa na jeraha ambalo likasababisha kutokwa na damu.

Huenda labda ukawa nyumbani unafanya shughuli zako na bahati mbaya ukajikata na kisu na kusababisha jeraha au chochote kile kikakufanya kupatwa na jeraha basi usipate shida fanya haya yafuatayo:

Kwanza tambua kwamba unapopatwa na jeraha huweza kuwa moja ya njia ya kusababisha kupatwa na maambukizi mengine kupitia jeraha hilo hivyo ni vyema ukazingatia haya yafuatayo kila unapopatwa na jeraha.

Asali
Asali ni moja ya suluhisho nzuri pale unapopatwa na jeraha unachopaswa kufanya paka kiasi cha asali kwenye jeraha hii itasaidia kukuepusha kupatwa hata na maambukizi mengine kupitia jeraha lako.

Aloe Vera
Pia unaweza kutumia aloe vera  unachotakiwa kufanya ni kutafuta tawi la mmea wa aloe vera kisha likate na mara baada ya kukata utapata ule utomvu wake kisha utapaka sehemu uliyopatwa na jeraha lako na itakusaidia kupata uponyaji. rudia kufanya hivyo kila baada ya muda.

Ukwaju.
Ukwaju ni njia nyingine ya kukabiliana na majeraha madogo madogo (vidonda) na huu ukwaju huweza kusaidia kuzuia utokaji wa damu zaidi kwenye jeraha. 

Kwa ufafanuzi zaidi tupigie simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment