Friday, 16 October 2015

KITUNGUU SI KIUNGO CHA MBOGA TU! LAKINI NI TIBA PIA ZIFAHAMU HAPA FAIDA ZAKE

Kitunguu maji ni moja ya kiungo ambacho wengi wetu hukitumia sana  karibu kila siku, hasa katika shughuli za jikoni, lakini kiungo hiki pia ni tiba kwa matatizo ya afya zetu.

Mtaalamu wa tiba asili Tabibu Abdallah Mandai anaeleza kwamba, unapotwanga gramu thelathini ikiwa na pilipili manga saba na kisha kumpatia mgonjwa mwenye tatizo la kutapika na kujisikia vibaya pamoja na kuharisha humsaidia sana kupona.

Tabibu Mandai anaendelea kueleza kwamba kwa wale wenye shida ya haja ndogo (mkojo) kuuma anaweza kuponda kiasi cha gramu sita ya vitunguu na baadaye kuchemsha katika nusu lita ya maji na kuiacha ichemke hadi pale itakapo pungua nusu ya ule ujazo wote kisha apatiwe mgonjwa anywe.

Aidha, mtaalam huyo anabainisha kwamba matone ya maji ya kitunguu ni dawa ya sikio na kusaidia kuondoa milio yote ya sikioni na tatizo hilo litaacha.

Mbali na hayo matatizo mengine yanayoweza kutatuliwa na kiungo hiki ni pamoja na kikohozi, vidonda vya tumbo, ngozi, figo pamoja na tumbo, ambapo Tabibu Mandai anasema kuwa, kwa tatizo la kikohozi kinachotakiwa kufanyika ni kuchukuwa kitunguu maji kimoja kikubwa na ukikate kate kwenye maji kisha chemsha maji hayo kwa dakika tano na baadaye mgonjwa anywe kijiko kikubwa kimoja kutwa mara tatu yaani asubuhi mchana na jioni.

Kwa ushauri zaidi mpigie simu Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment