Friday, 2 October 2015

KUELEKEA KUMBUKUMBU YA MWL. NYERERE, LEO TUPATE WOSIA HUU KUHUSU UDINI NA UKABILA

Kila inapofika Octoba 14 ya kila mwaka Tanzania huadhimisha kumbukumbu ya kufariki kwa muasisi na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere aliyefariki Octoba 14, 1999.

Mwalimu Nyerere hukumbukwa na Watanzania wengi kwa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na uadilifu wake,  lakini kubwa zaidi ni ile falsafa yake ya umoja ambayo ilipelekea kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar na kujenga umoja kwa wananchi pia.

Kuna mambo mengi ambayo Mwlm Nyerere aliyasimamia sana enzi za uhai wake, ikiwa ni pamoja na kukemea swala la udini na ukabila.

Hapa napenda kukuletea hii video fupi ya Mwalimu Nyerere akizungumza kuhusu mambo ya udini na ukabila hususani katika nyakati za uchaguzi kama tulizonazo sasa kuelekea Octoba 25.

No comments:

Post a Comment