Thursday, 8 October 2015

KUNA SABABU 5 ZINAZOKUFANYA USIFANIKIWE KATIKA MAISHA YAKO KIJANA, ZIFAHAMU HAPA LEO


Hujambo mdau wangu wa www.dkmandai.com kwa sasa napenda tubadilishane mawazo ya kimaisha zaidi ambayo yatatusaidia kwenda mbele kiuchumi zaidi.


Najua kuna vijana wengi tupo mtaani tunahangaika kutafuta maisha kila siku kwa lengo la kufikia mafanikio fulani, jambo ambalo ni nzuri sana, lakini kuna baadhi yetu huenda tusiweze kufika kwenye hayo mafanikio kutokana na vitabia fulani fulani.

Sasa wacha tutumie muda huu kufahamishana baadhi ya mambo ambayo yanaweza kusababisha tukashindwa kufikia ndoto zetu:-

Kushindwa kuwa na ufanisi
Wengi wetu tunafanya kazi kwa bidii sana na kila siku tunaamka asubuhi na mapema kuelekea maeneo yetu ya kazi, lakini shida inakuja pale tunapofika kwenye kazi zetu hatuna kabisa ufanisi kwa kifupi tunafanya kazi kwa mazoea hii ni mbaya na kama unahitaji mafanikio ni lazima ubadilishe utaratibu huo unachotakiwa kufanya sasa si  tu  kufanya kazi kwa bidii, bali  ufanye  kazi nadhifu.

Hatujui kutumia muda wetu
Vijana wengi kwa sasa wanapoteza muda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii, ingawaje si vibaya kucheki kile kinachoendelea facebook, Instagram na mitandao mingine pia kama hiyo, lakini ni lazima tukumbuke muda tunaotumia kulike status na picha za watu huwa hazituongezei chochote kwenye maisha yetu na badala yake tunapoteza muda tu, hivyo ni vyema tuzingatie matumizi ya muda na tuutumie muda kufikiri mambo ya kujiongezea kipato zaidi.

Kukata tamaa haraka
Vijana wengi pale wanapoona mambo yameenda tofauti na matarajio yao basi hukata tamaa mapema na husaau kuwa ili kufikia mafanikio kunahitajika uvumilivu, kiukweli hakuna mtu yeyeyote mwenye mafanikio leo ambaye aliyapata kirahisi ukweli ni kwamba wengi walipambana kimaisha na hawakukata tamaa hata pale walipozongwa na magumu kuelekea kwenye mafanikio yao, hivyo nikusihi acha kukata tamaa fanya kazi kwa bidii utafika unapopata huku ukimuomba Mungu pia.

Kuogopa kushindwa (take risk)
Watu wengi huhitaji kufanya kitu fulani ambacho wanaamini kitakuwa na manufaa kwao, lakini baadaye hujikuta wakishindwa kuyaona manufaa kwa sabababu ya kuogopa kushindwa, wengi wanapoanzisha kitu huwaza itakuaje endapo watashindwa. sasa kwa mtu anayetaka mafanikio siku zote huwa hawazi kushindwa na mara zote huwaza kufanikiwa na hata akishindwa huwa achoki kurudia hadi kuona mwisho wake. Hivyo na wewe kijana ni vyema ukaanza kuwa na moyo huo leo.
Kushindwa kuzitumia fursa
Kuna wakati katika jamii tunazoishi huwa kunafursa zinajitokeza, lakini watu huogopa kuzitumia sasa ni vizuri ukajua kuwa siku zote mtu anayehitaji kufanikiwa ni lazima atazame mazingira ya fursa na kujua namna ya kuyachukua na kwenda nayo kwenye mafanikio ya kimaisha.
Hayo ni baadhi ya mambo muhimu ambayo naamini ukiyafuata basi huenda utafanikiwa katika kile unachokifanya na hatimaye kuyafikia malengo yako ya kimaisha hususani ya kiuchumi kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment