Monday, 5 October 2015

KUTANA NA HII SHERIA MPYA YENYE LENGO LA KUTHIBITI MIFUKO YA PLASTIKI

Si jambo jipya kusikia wataalam wa mazingira wakilalamika kuhusu mifuko ya plastiki kuleta uharibufu kwenye mazingira, na ishu ya mifuko hii ilishawahi kufika hadi kwenye Bunge la Tanzania na kujadiliwa ambapo wabunge walilalamika kuhusu mifuko hiyo kuathiri mazingira.

Kumbe hata nchini Uingereza nao wanakerwa na mifuko hiyo ya plastiki na wao wameamua kutengeneza sheria mpya ambayo imependekeza kwamba kila mfuko wa plastiki utauzwa kuanzia Pound 5 ambazo kwa pesa yetu ya Tanzania ni kama Tshs. 16,400/= 

Uingereza wameamua kuweka bei hiyo, huku wakiamini kwamba bei ya mifuko ikiwa juu kiasi hicho, watumiaji wa mifuko hiyo watakuwa wachache na haitozagaa tena mitaani.

Kwa mujibu wa tafiti za mwaka 2014 zilionesha jumla ya mifuko ya plastiki bilioni 7.6 ilitolewa kwa wateja kutoka kwenye Supermarkets za Uingereza, hiyo ni sawa na kila mtu mmoja alipatiwa jumla ya mifuko 140.

Hata hivyo kufuatia gharama hizo za mifuko itasaidia watu kukumbuka kubeba mifuko yao kutoka nyumbani wanapoenda Supermarket ili kuokoa Tshs. 16,400/= ambayo wangeilipia kwa kununua mfuko mmoja tu wa kuwekea bidhaa wanazonunua.

No comments:

Post a Comment