Saturday, 24 October 2015

LEO KUNA HAYA MAMBO MUHIMU KUHUSU PAPAI KUSAIDIA AFYA YA NGOZI

Leo ni weekend jamani ni vyema tuangazie kuhusu masuala ya afya ya ngozi na urembo kwa ujumla.

Kwa kawaida binadamu yeyote mwenye akili timamu mara zote hupenda kuonekana nadhifu na mtanashati, 

Miongoni mwa mambo ambayo huweza kumuweka mtu kuonekana vizuri ni pamoja na suala la kuwa na ngozi nzuri.

Leo nimeona ni vyema nikakupatia huu uwezo wa papi katika kukufanya ukaonekana vizuri hasa kwenye ishu ya ngozi. 

Papai ni tunda ambalo linauwezo wa kurejesha au kuziba sehemu za ngozi zilizoumia, papai pia hung'arisha ngozi.

Ili papai likusaidia kwenye ngozi yako unashauriwa kuchukua papai lenyewe lililoiva kisha changanya na asali paka usoni kisha kaa nalo kwa muda wa dakika 10 baadaye safisha, fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaona mabadiliko katika ngozi yako.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment