Wednesday, 14 October 2015

LEO NI NYERERE DAY, PATA NAFASI YA KUSIKIA HAPA WOSIA WAKE KUHUSU MASUALA YA UCHAGUZI WA KIONGOZI BORA (VIDEO)

Hayati Mwlm Julius Kambarage Nyerere
Kila inapofika siku kama ya leo Octoba 14 ya kila mwaka  Tanzania huadhimisha kumbukumbu ya kufariki kwa muasisi na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere aliyefariki Octoba 14, 1999.

Ikiwa sasa ni miaka 16 tangu Mwalimu Nyerere alipotutoka lakini Watanzania bado wanamkumbuka kwa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na uadilifu wake,  lakini kubwa zaidi ni ile falsafa yake ya umoja ambayo ilipelekea kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar na kujenga umoja kwa wananchi pia.

Kuna mambo mengi ambayo Mwlm Nyerere aliyasimamia sana enzi za uhai wake, ikiwa ni pamoja na kukemea swala la udini na ukabila smbamba na vitendo vya rushwa na uchu wa madaraka pia

Sasa ikiwa leo ni Oktoba 14 siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwlm Julius Kambarage Nyerere nimeona nikuwekee hii video fupi ya Mwalimu Nyerere akizungumza kuhusu mambo ya udini na ukabila hususani katika nyakati za uchaguzi kama tulizonazo sasa kuelekea Octoba 25 na ikiwa hadi sasa tumebakiza siku 11 tu kufikia siku ya uchaguzi mkuu.


No comments:

Post a Comment