Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 31 October 2015

LEO TABIBU MANDAI ANAELEZA KUHUSU DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA

Tabibu Abdallaha Mandai Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbalist Clinic

Leo Jumamosi tulifahamu baaadhi ya sababu ambazo huchangia kutoka kwa mimba mara kwa mara, lakini nimeona ni vyema sasa tufahamu dalili za kutoka kwa mimba kwa mama mjamzito.

Mambo mengi hususani haya ya kiafya yanapotokea kwenye miili yetu mengi huonesha viashiria yaani dalili, lakini tatizo kubwa linakuja wengi wetu huwa hatufahamu viashiria vya matatizo mbalimbali ndani ya miili yetu na ndio maana huwa tunajikuta tunagundua matatizo baada ya muda mrefu mrefu kupita, ambapo tayari tatizo linakuwa kubwa tayari.

Sasa ni vyema kwa sasa tuzifahamu hizi dalili ambazo huweza kuonekana kwa mwanamke mwenye ujauzito ambaeye mimba inakuwa imetoka kama ifuatavyo>>

Moja ya kiashiria cha tatizo hili ni mwanamke kuanza kutokwa na damu nyepesi sehemu za siri

Aidha, mwanamke pia huweza kuanza kutokwa na damu nzito yenye mabonge mabonge sehemu za siri

Pia mama huweza kuhisi maumivu makali sana ya tumbo ambayo huweza kuambatana na maumivu ya kiuno pamoja na kuendelea kutoka kwa dmau nyepesi shemu za siri.

Ukiona dalili hizo ni vizuri ukafanya haraka sana kuwahi kwenye kituo cha afya amavcho kipo karibu na wewe ili wataalam wajue namna ya kukusaidia. Usikubali hata kidogo kuendelea kubaki nyumbani unapokumbwa na dalili hizo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment