Monday, 19 October 2015

MAAJABU MENGINE YA KUTUMIA KINYWAJI CHENYE MCHAICHAI

Mchai chai ni mmea ambao unatambulika hapa nchini pamoja na Afrika kwa ujumla wake na umekuwa ukitumika kuongeza ladha kwenye chai.

Naamini kwamba wengi wetu tumekuwa tukiutambua mmea huu kama kiungo katika chai ambacho husaidia sana kuleta harufu nzuri zaidi katika chai.

Siku zote tumekuwa tukitoa nafasi kwa wadau wetu kuuliza maswali mbalimbali kupitia ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic -mhc pamoja na namba zetu za simu za 0716 300 200, 0769 400 800 na unapouliza huko basi majibu utaweza kuyapata mara moja.

Leo napenda kujibu swali la mdau wetu ambaye alihitaji kujua endapo kuna tiba asili yenye uwezo wa kuponya tatizo la miguu kuvimba na unachopaswa kufanya endapo unatatizo hilo ni kutafuta majani ya mchai chai kisha yachemshe na uchuje halafu kunywa maji hayo kila siku jitahidi kwa siku umalize lita moja na utaona mabadiliko. 

Lakini mbali na faida hiyo kwa pia mmea huo husaidia kukabiliana na tatizo la baridi yabisi, kusafisha figo na kuwasaidia wale wenye shida ya matumbo kuunguruma na hivyo kumsaidia mhusika kurejea katika hali ya kawaida.

Kama utahitaji maelezo zaidi au ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu ni vyema ukafanya uamuzi sahihi wa kufika Mandai Herbalist Clinic ili kuonana na Tabibu Abdallah Mandai na kuweza kupata matibabu sahihi. Unaweza kupiga simu namba; 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika moja kwa moja ofisini Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment