Thursday, 1 October 2015

MAHUSIANO NAYO YANAUMUHIMU WAKE, LEO TUJUZANE KUHUSUNAMNA YA KURUDISHA UPYA MAHUSIANO YALIYOVUNJIKA

Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com, leo napenda tuguse kidogo masuala ya mahusiano kwani nayo yanaumuhimu wake katika maisha yetu ya kila siku.

Nitapenda kuzungumzia mambo muhimu ya kufanya pale inapotokea ulikwaruzana na mpenzi wako sasa unahitaji kuyarudisha mahusiano yenu upya:-

KUOMBA MSAMAHA.
Msamaha ni jambo la msingi na muhimu katika masuala haya ya mahusiano, hivyo inapotokea unahitaji kurudisha mahusiano yako ya awali kwanza lazima ukiri makosa yako uliyofanya hapo mwanzo hadi kuperekea mikwaruzano yenu na baada ya kukiri ni vyema ukaomba msamaha ili kuanza upya tena na kusahau makosa yaliyotendeka hapo awali.

MABADILIKO
Lazima ujitathimini kuhusu yale makosa yaliyofanya mkakosana na mwenzi wako na baada ya kuyajua utapaswa kufanya mabadiliko ili yasijirudie tena katika mahusiano yenu, kwa kufanya hivyo mahusiano yenu yataimarika na kuwa na nguvu zaidi ya hapo awali.

ONESHA KUJUTA.
Unapohitaji kurudiana na mwenzi wako mliyekosana ni lazima uonekane kuwa unajutia kwa kukosana naye, hali hiyo utapaswa kuionesha kuanzia usoni hadi moyosi yaani kihisia uonekane kuwa ni yule mtu anayejuta.

Hayo ni machache kuhusu masuala ya mahusiano, lakini kwa ushauri zaidi kuhusu afya na magonjwa mbalimbali tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment