Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 27 October 2015

MAMBO 5 MUHIMU YATAKAYOKUFANYA UENDELEE KUWA NA AFYA BORA ZAIDI


Siku zote ili kufikia malengo yoyote katika maisha afya bora ni mhuimu sana sasa hpa napenda tuangazie mambo muhimu 5 ya kuzingatia ili kudumisha afya yako.

Pata lishe bora
Chakula ni muhimu sana kwa afya na ni chanzo kikubwa cha afya bora pia. hata hivyo chakula pia kinaposhindwa kutumika vizuri au kwa utaratibu unaofaa huweza kuwa ni chanzo cha magonjwa mengine.

Jinsi unavyopangilia mlo wako huweza kukufanya uwe na afya bora au kubomoa kabisa afya yako, hivyo ni vyema kuwa makini na chakula chako. Kama tunavyosisitiza siku zote pendelea kula mboga za majani, vyakula vilivyo na virutubisho asilia na kunywa maji mengi kila siku.

Fanya Zoezi

Mazoezi yana kazi kubwa ya kuufanya mwili kuwa na afya imara na bora, kwani mazoezi husaidia sana kuongeza mzunguko wa damu mwilini vilevile mazoezi ni muhimu kwa mtu yeyote ili kuufanya mwili uwe katika afya njema.Tengeneza ratiba ya kufanya mazoezi angalau hata mara mbili tu kwa wiki hii inatosha sana kwa kuanzia.

Pata mapumziko
Afya inahusisha vitu vingi, lakini kupumzika ni kitu muhimu pia,mtu ambaye hukosa muda wa kupumzika kwa kiasi kikubwa huathirika na kupunguza uwezo wake wa ufanisi kwenye mambo mbalimbali au shughuli zake za kila siku na hivyo kuchangia mhusika kushindwa kufikia malengo yako.

Achana na ulevi
Pombe ni hatari hasa kwa wale wanaoiendekeza katika maisha yao na kama ikinywewa kupitiliza. huweza kuleta madhara makubwa kwa afya ya binadamu, lakini bila kusahau na sigara vilevile ni hatari pia.

Jaribu kufunga kula na kunywa
Afya siyo kula tu bali hutegemeana na kujinyima pia. Vyakula vingi tunavyokula hutuletea sumu ndani ya miili yetu hivyo unapofunga kwa hapo utakuwa umeusaidia sana mwili kuondoa uchafu na kujisafisha na kuwa na afya bora zaidi. Hivyo, ni vizuri kuwa na muda wa kufunga kila mara ili kuweza kuboresha afya.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment