Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 1 October 2015

MANENO YA DC MAKONDA KUHUSU HALI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Ugonjwa wa kipindupindu umeendelea kuripotiwa jijini Dar es Salaam , kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda September 30, 2015 alitembelea baadhi ya maeneo ndani ya Wilaya ya Kinondoni eneo la Mikocheni ambako kuna Garage za Magari pamoja na Viwanda vidogovidogo kuangalia hali ya mazingira ilivyo katika maeneo hayo.

Inaelezwa kuwa idadi ya wagonjwa waliolazwa hospitali kutokana na ugonjwa huo inatajwa kuongezeka, hiyo ni moja ya sababu iliyofanya Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda kupita maeneo hayo na kutoa tahadhari.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda 
Akizungumza na vijana aliokutana nao wakiwa katika mazingira yao ya kazi DC Makonda aliwataka  kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa huo wa kipindupindu.

“Jitahidi hata kama uko kwenye mazingira magumu hakikisha unalinda afya yako, iko njia hata kwenye mazingira magumu kutunza afya yako” alisema DC Paul Makonda.
No comments:

Post a Comment