Wednesday, 14 October 2015

MPENDE MWANAO ANZA SASA KUMLISHA VYAKULA HIVI ILI AWE NA AFYA BORA ZAIDI

Naamini kwamba kila mzazi siku zote hupenda kumuona mtoto wake akibaki kuwa mwenye furaha na mwenye afya njema na siku zote chakula bora na chenye virutubisho ndio moja ya vitu muhimu sana katika ukuaji wa mtoto.

Kwa kawaida wakati wa hatua za ukuaji wa mtoto mwili wake huhitaji sana vitamin za kutosha pamoja na madini kwa ajili ya maendeleo ya afya yake.

Lakini kutokana na harakati za maisha familia nyingi hujikuta hawazingatii sana maandalizi ya vyakula vyenye virutubisho vya kutosha kwa watoto wao na hapa tunazungumzia wale watoto ambao tayari wameshafikisha umri wa kuweza kumudu kula vyakula vingine mbali na maziwa ya mama

Vifuatavyo ni miongoni mwa vyakula muhimu kwa mtoto ambavyo vitamfanya kuendelea kukua vizuri 
Maziwa
Kwa kawaida maziwa ni mazuri mno kwa watoto, ndani ya maziwa kuna madini ya calcium na phoshorous ambavyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya afya ya mifupa, meno na kucha.

Maziwa pia ni chanzo kizuri cha protin, vitamin A, B2 na B12 ambavyo vyote ni muhimu kwa afya ya mtoto.
Viazi vitamu
Viazi hivi ndani yake vina kitu kiitwacho beta carotene na carotenoids ambavyo vyote ni muhimu sana kwa afya ya macho, lakini pia ni chanzo kizuri cha vitamin A, C, E bila kusahau madini chuma, nyuzinyuzi 'fiber' na 'calcium', ambavyo vyote huapatikana ndani ya viazi
Mayai
Mayai ni mazuri sana kwa ukuaji wa mtoto, kutokana na kuwa na protini ya kutosha ambayo ni muhimu sana kwa ukuaji wa watoto.

Mayai pia yanautajiri wa vitamin B ambayo inakazi kubwa katika maendeleo ya ubongo na utendaji kazi wake.

Maziwa mtindi
Maziwa haya yana bakteria wazuri ambao ni muhimu kwa kujenga uwezo wa kinga za mwili kuimarika zaidi, lakini pia huweza kumsaidia mtoto katika mfumo wake wa umeng'enyaji wa chakula tumboni kuwa mzuri zaidi.

Unapompatia maziwa mtindi mtoto kila siku, tambua kuwa utakuwa unamjengea uimara wa afya ya mifupa pamoja na meno.

Najua katika hii ya maziwa mtindi huenda ikawa ngumu kwani watoto waliowengi huwa hawafurahishwi sana na ladha ya mtindi, hivyo ukiona mtoto hataki basi jaribu kitu kingine kati ya vyote vilivyoainishwa.

Kwa maelezo zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment