Thursday, 15 October 2015

MWILI WA MAREHEMU DK KIGODA UMEAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM (PICHA)


Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania, Dk. Abdallah Omar Kigoda aliyefariki nchini India wakati akipatiwa Matibabu umeagwa leo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya viongozi wakuu wa serikali waliofika kuaga mwili wa marehemu Dk. Kigoda
Mwili huo ulifikishwa mapema leo katika Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam ambapo watu mbalimbali wakiongozwa na baadhi ya Viongozi wa Juu wa Serikali, ndugu na jamaa wametoa heshima za mwisho na kumuaga marehemu Dk. Kigoda, na baadaye kufuatiwa na safari kuelekea Tanga kwa ajili ya mazishi.

Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry akiwa na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam pamoja na Makamu wa Rais Dk Ghalib Bilali wakimswalia Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, wakati wa swala hiyo iliyoswaliwa kwenye Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo asubuhi


Mwili wa marehemu Dk Kigoda unatarajiwa kuzikwa leo jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga. 


"Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani Marehemu Dk Kigoda amin RIP"

No comments:

Post a Comment