Monday, 5 October 2015

NJIA HIZI ZITAKUFANYA KUENDELEA KUWA NA AFYA BORA KATIKA MAISHA YAKO YOTE

Kila mtu hupenda kuishi akiwa na afya bora na siku zote afya bora huchangiwa na vyakula ambavyo tunakula kila siku.

Lakini si chakula pekee huweza kuimarisha afya yako, pia kuna mambo mengine ambayo ni sehemu ya kuimarisha afya zetu.

Ili kuwa na afya njema ni vizuri kupata nafasi ya kupumzika, tukizungumzia kupumzika ni kupata nafasi ya kulala kiasi cha kutosha, usingizi ni sehemu muhimu sana katika afya. Usingizi una nafasi kubwa sana kwa faida ya afya ya akili/ubongo wetu. Pia ni vyema ikafahamika kuwa mapumziko husaidia mwili kujijenga vizuri zaidi.

Fanya mazoezi angalau mara tatu katika wiki, kwa kufanya hivyo husaidia kukukinga na magonjwa ya hapa na pale hususani yale magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Muhimu hapa ni kuchagua aina ya mazoezi unayoyaoendana nayo, kumbuka kwamba mazoezi ni muhimu kwa kila mtu.

Asilimia 60% ya miili yetu imetengenezwa au imesheheni maji, hivyo maji yanahitajika kwa ajili ya kuondoa takataka au vitu visivyofaa ndani ya miili yetu ili kuimarisha afya zetu zaidi.

Aidha, ili kujenga afya bora unapaswa kujenga utaratibu wa kutumia matunda kwa wingi, kwa sababu matunda ni mojawapo ya chanzo kizuri cha vitamin na madini mbalimbali mwilini. Hivyo ni muhimu kuzingatia ulaji wa matunda kwa wingi kila siku.

Kwa kulinda zaidi afya yako ni vizuri kujiepusha pia na tabia hatarishi kama vile kushiriki ngono zembe, ulevi pamoja na uvutaji sigara kwani hivyo vyote kwa pamoja husababisha kudhorotesha afya yako.

Ikiwa unahitaji ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment