Wednesday, 14 October 2015

PATA NAFASI YA KUFAHAMU HAYA MAAJABU YA MAFUTA YA NAZI NA NDIMU


Kinadada wengi huangaika mara kwa mara kwa lengo la kuhitaji kuwa na nywele nzuri zenye muonekano mzuri kila siku, lakini kwa bahati mbaya sana si wote wanabahatika kufanikiwa kuwa na nywele hizo nzuri.

Si ajabu kabisa kumsikia mwanamke akisema ameshakata tamaa kutokana na mwenendo wa makuzi ya nywele zake kutokwenda vizuri na wengi hukata tamaa mara baada ya kutumia dawa mbalimbali za kukuza nywele lakini hujikuta wakikosa hayo mafanikio na baadhi yao hujikuta nywele zinazidi kuisha zaidi au kudumaa.

Kama wewe ni dada ambaye huenda unashida hiyo basi tambua kwamba moja ya sababu ya nywele kushindwa kukua vizuri ni pamoja na hii sababu ya kuwa na mba kichwani mwako.

Sasa leo napenda kukupatia hii mbinu ya kumaliza shida ya mba kwa kutumia mchanganyiko wa mafuta ya nazi na  ndimu ili baadaye uweze kuwa na nywele zenye afya bora.

Jambo la kufanya kwanza kabisa utahitajika kuziosha nywele zako vizuri kabisa na uzikaushe kisha tafuta mafuta ya nazi ndimu.

Weka mafuta ya nazi kwenye kibakuli kisha pimakijiko kimoja cha  chakula chenye maji ya ndimu na ukoroge vyema. Kisha tumia mchanganyiko huo kwa kuweka kichwani na uhakikishe unafika hadi kwenye mizizi ya nywele kabisa fanya hivyo kwa dakika kadhaa. Kisha kaa na mchanganyiko huo bila kuosha kichwa kwa dakika kama 20 hivi.

Baada ya dakika hizo kupita osha kichwa chako vizuri, kisha ufanye zoezi hilo kwa mara mbili hadi tatu kwa wiki ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Ikiwa unahitaji kuuliza zaidi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au fika ofisini kwetu tupo Ukonga, Mombasa maeneo ya Mongolandege jijini Dar es Salaam 


No comments:

Post a Comment