Saturday, 3 October 2015

RAIS KIKWETE KUHUTUBIA BUNGE LA KENYA

Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuhutubia bunge la Kenya Jumanne wiki ijayo huku akielekea kujiandaa kuondoka mamlakani.

Rais Kikwete atahutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti katika majengo ya bunge jijini Nairobi.

Rais Kikwete atakuwa kiongozi wa pili wa taifa la nje kuhutubia bunge Kenya baada ya aliyekuwa kiongozi wa Nigeria Goodluck Jonathan kuwa kiongozi wa kwanza kuhutubia bunge la Kenya Septemba 6, 2013.

Spika wa Bunge la Kitaifa Kenya Justin Muturi aliambia wabunge Alhamisi kwamba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amemwandikia akiomba ruhusa kiongozi huyo mwenzake akubaliwe kuhutubia.

“Ningependa kuwajulisha kwamba, baada ya kufanya mashauriano, Spika wa Seneti nami tumekubali ombi hilo,” Bw Muturi aliwambia wabunge.

Kwa muda sasa, Rais Kikwete amekuwa akizunguka maeneo mbalimbali ya Tanzania akiwaaga wananchi. Pia Rais Kikwete atakuwa kiongozi wa kwanza kuhutubia bunge la taifa jingine Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment