Thursday, 15 October 2015

RAIS KIKWETE: MSICHAGUE VIONGOZI WENYE VIGUGUMIZI VYA KUSEMA RUSHWA NI MBAYA


RAIS Jakaya Kikwete amesisitiza wapiga kura katika uchaguzi mkuu, kumchagua mgombea urais asiye na kigugumizi kwenye kukemea rushwa.

Akizungumza jana mjini Dodoma kwenye kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru sambamba na kumbukumbu ya miaka 16 ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere, yaliyofanyika mjini Dodoma, Rais Kikwete alisema baadhi ya viongozi kwenye vinywa vyao, wana vigugumizi vya kutaja neno rushwa na wanapata tabu nalo.

“Tunataka viongozi wasio na vigugumizi kusema rushwa ni mbaya,” alisema Rais Kikwete

Aidha, Rais Kikwete alisema kumchagua kingozi mwenye kigugumizi na rushwa ni kutafuta majanga na watanzania wanatakiwa kufanya maamuzi ya kuwakataa, wasichaguliwe kuwa viongozi.

Pamoja na hayo Rais Kikwete aliwataka wananchi kufuata maagzio yote yaliyoagizwa na NEC

“Msikubali kuchuuzwa na viongozi wenu, hizo ni vurugu, tunaomba agizo la NEC liheshimiwe, atakayekaidi hatutamvumilia, na msilazimishe serikali kufanya yasiyopenda, lisilobudi lisifanywe”alisisitiza Rais Kikwete.

Akifafanua zaidi kuhusu hilo Rais Kikwete alisema haina maana kulinda kura huku wewe uko nje ya kituo cha kura.

“Hivi unapoambiwa usiondoke ubaki kituoni kulinda kura, mantiki yake ni rahisi wewe uko nje ya kituo cha kura, huwezi kulinda kura, ila walio ndani ndio wanaolinda na hao ni mawakala, sasa nyie wengine uko nje ni kuleta vurugu”,alisema Rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment