Friday, 16 October 2015

STORI KUHUSU EBOLA ZIMERUDI TENA WALIOWAHI KUATHIRIKA WATAKIWA KUTUMIA KONDOMUWaathiriwa wa ugonjwa wa Ebola wametakiwa kutumia mipira ya kondomu hadi kutakapokuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu matokeo ya utafiti yanayoonesha kwamba virusi hivyo husalia katika majimaji ya mbegu za kiume kwa kipindi cha hadi miezi tisa.

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa maambukizi ya ebola kupitia tendo la ngono ni kidogo mno na kutaja maeneo ya taifa la Sierra Leone ambayo yana idadi kubwa ya manusura lakini hayana visa vipya vinavyojirudia.

Lakini mkuu wa WHO Margeret Chan ameiambia BBC kwamba kuna maswali mengi.''Hatujui iwapo wanaweza kuambukiza ama vipi ,bado hatuna ushahidi wa kutosha''.

''Kiwango cha ufahamu bado kinatutia wasiwasi ,ndio maana lazima tuchukue tahadhari, kwa hivyo tunawashauri manusura kujilinda kupitia mipira''.

No comments:

Post a Comment