Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 6 October 2015

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI KUHUSU MAUAJI YA AFISA POLISI DAR ES SALAAMAgosti 4, 2015 yalifanyika mauaji ya ASP Elibariki Pallangyo nyumbani kwake maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam, tukio hilo lilifanywa na majambazi.

Sasa Oktoba 05, 2015 Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza kuwakamata majambazi sugu sita walioshiriki katika mauaji hayo.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda Suleiman Kova amesema "Watu sita wanashikiliiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuuwa afisa wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro ASP Elibariki Palangyo ambaye alikuwa mkuu wa kikosi cha kupambana na uhalifu hasa ujambazi wa kutumia silaha kule Morogoro"

Kamanda Kova alisema "Afisa huyo alikuja Dar es Salaam kuiona familia yake, lakini usiku wa tarehe 4 mwezi wa nane alivamiwa na majambazi 6 nyumbani kwake Temeke na kuuliwa mbele ya familia yake, tukiwa kama jeshi la polisi tuliweza kufanya upelelezi na tumefanikiwa kuwakamata wahutumiwa wanaohusika na tukio hilo"
"Tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita wanaohusika na tukio hilo la kumuuwa afisa huyo wakati wa kuhojiwa watuhumiwa hao walikiri kuwa ni kweli walihusika na tukio hilo la kumuuwa afisa polisi wa mkoa wa Morogoro" alisema Kamanda Kova

Akiwataja waliokamatwa Kamanda Kova alisema ni Omary Salehe maarufu kama 'bonge mzito' (39) ambaye ni mkazi wa Mtoni mtongani ambaye ni Kiongozi wa kundi hilo.

Kamanda Kova alisema wengine waliokamatwa ni Saidi Saidi Mazinge (37) mkazi wa Tegeta Kibaoni, Rashidiwa Tsonb maarufu dodo (21) mkazi wa Vingunguti, Ramadhani Salum maarufu nguzo (38) mkazi wa Mbagala Kibugurwa, Bakari Salim Rashid maarufu Malenda (38) mkazi wa Mbagala Kizuiani pamoja na Hamisi Hamisi maarufu Freemason (24) Mkazi wa Mbezi Mwisho.

Hata hivyo mtuhumiwa namba mmoja Omary Salehe maarufu bonge mzito alikutwa na silaha bastola aina ya revolver iliyofutwa namba na baada ya mahojiano. Mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu kabla ya kufariki alijaribu kuwatoraka askari kwa kukimbia alijeruhiwa na hatimaye alifia njiani wakati akipelekwa hosptalini. Pia inasemekana marehemu alipotezana na familia yake miaka mitani iliyopita akiwa kwenye harakati ya ujambazi.

No comments:

Post a Comment