Thursday, 1 October 2015

TABIBU MANDAI LEO ANAKUFAHAMISHA KUHUSU MADHARA YA UGONJWA WA KISUKARI NA JINSI YA KUISHI NAO VIZURI


Ugonjwa wa kisukari ni hali ambayo hutokea pale ambapo kiwango cha sukari mwilini huzidi kuliko mahitaji ya mwili kwa kawaida ni muhimu kuzingatia kudhibiti sukari mwilini.

Unaweza kudhibiti halu hiyo kwa kupata mlo kamili, kudhibiti uzito wa mwili wako, kufanya mazoezi na kufanya uchunguzi wa sukari yako mwilini mara kwa mara.

Sukari inaposhindwa kudhibitiwa mwilini, huharibu mishipa ya damu na fahamu na kuathiri kinga ya mwili na hivyo mwili hushindwa kupambana na maambukizi.Hali hiyo huweza kupelekea mhusika kupata vidonda au maambukizi na maambukizi hayo huweza kuchelewa kupona tofauti na mtu wa kawaida. 

Kwa hiyo ni muhimu sana kuhakikisha unadhibiti kiwango cha glukozi kwenye damu kwa kuzingatia mabadiliko katika lishe na mazoezi pia.

Aidha,  miguu, ngozi, fizi na macho ni kati ya viungo ambavyo hushambuliwa sana na ugonjwa huu wa kisukari, sasa ni vyema kujikinga na kuzuia au kuvitunza viungo hivyo na kukagua mara kwa mara ili kuepuka madhara hayo.

Unapokuwa tayari una kisukari ni vyema ukazingatia kuhakikisha unakagua miguu yako vizuri kila siku, safisha miguu yako kwa maji safi na uikaushe vizuri kwa taulo safi.

Jikague mara kwa mara kama unakidonda, mchubuko au fangasi ikiwa kuna shida yoyote basi onana na daktari wako mara moja

Pia unapaswa kujenga utaratibu wa kupaka mafuta ya kutosha ngozi yako ili isiwe kavu, pia zingatia kutotembea bila viatu na unapovaa viatu basi vaa viatu vinavyokukaa vizuri usivae viatu vinavyokubana au kukuumiza.

Kwa ushauri zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment