Monday, 26 October 2015

UKIONA UNAKOSA HAMU YA KULA KILA SIKU BASI JUA UTAKUWA NA TATIZO TUMIA VITU HIVI VITAKUSAIDIA

Ishu ya kukosa  hamu ya kula inaweza kumkuta mtu yeyote na wakati wowote na mara nyingi hali hii huchangiwa na sababu kadhaa ikiwemo hali ya uchovu kupita kiasi.

Mtu anaweza kujikuta akikosa kabisa hamu ya kula kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya, au kuishi na wasiwasi, hofu, mawazo au majonzi.

Unapokosa hamu ya kula mara kwa mara huchangia sana mhusika kukonda na kupungua uzito pamoja na kushuka kwa kinga ya mwili hivyo kushambuliwa na maradhi kirahisi zaidi.

Hapa ninazo njia za kuepuka tatizo hilo la kukosa hamu ya kula kama ifuatavyo:-

Ili kukabiliana na tatizo hilo unaweza kutumia limao au chungwa ambavyo ndani yake kuna vitamin C ambayo huongeza hamu ya kula kwa mhusika, hivyounaweza kula matunda hayo au kutengeneza juisi yake ili kupata msaada zaidi.

Pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kwani husaidia sana kuamsha mfumo wa chakula na kufanya kazi vizuri na kuongeza hamu ya kula. hata hivyo kitunguu swaumu hicho unaweza kukitafuna au kuunga kwenye chakula.

Halikadhalika tangawizi nayo ni msaada mkubwa wa tatizo hili na huleta hamu ya kula kwa wale ambao hukosa kabisa hamu ya kula.

Hata hivyo ni vyema ikafahamika kuwa hili tatizo la kukosa hamu ya kula mara nyingine huwa ni kiashiria tosha kwamba mhusika anadalili za homa au kuna tatizo ndani ya mwili wake hivyo ni vyema kuwaona wataalam wa afya kwa uchunguzi zaidi

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment