Sunday, 4 October 2015

UMEIPATA HII TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU WATU WAREFU KUWA KATIKA HATARI YA KUPATWA NA SARATANIJe, wewe ni mrefu? sasa kama jibu ni ndio kutana na huu utafiti wa kampuni moja ya Sweben uliofanyiwa na watu milioni 5.

Kwa mujibu wa utafiti huo umethibitisha nadharia kwamba urefu wa mtu na hatari za ugonjwa wa saratani ni vitu ambavyo vina uhusiano.

Utafiti huo umebaini kwamba watu warefu wana hatari ya kushikwa na saratani ya matiti pamoja na ile ya ngozi pamoja na saratani nyingine.

Matokeo yake yalibaini kwamba kwa kila ziada ya sentimita 10,wakati mtu anapokuwa mtu mzima hatari za kushikwa na saratani huongezeka kwa asilimia 18 miongoni mwa wanawake na asilimia 11 miongoni mwa wanaume.


Lakini wataalam walisema kuwa utafiti huo haukuangazia hatari nyingine ambazo watu warefu hawafai kuwa na wasiwasi nazo.

Tafiti za awali zimeonesha kwamba uhusiano kati ya urefu wa mwanadamu na hatari za kushikwa na ugonjwa wa saratani,ijapokuwa haijulikani ni kwa nini.

Ripoti za awali za utafiti huo zilizowasilishwa katika mkutano wa wagonjwa wa watoto,watafiti kutoka taasisi ya Karolinska mjini Stockholm walielezea vile walivyolifuatilia kundi moja la watu wazima kwa zaidi ya miaka 50.


Wanawake warefu wana hatari kubwa ya hadi asilimia 20 ya kupatikana na saratani ya matiti huku wanaume na wanawake warefu wakiwa na hatari ya juu ya kupatikana na saratani ya ngozi kwa asilimia 30.

No comments:

Post a Comment