Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 22 October 2015

USIKUBALI KUSHIKA UJAUZITO KABLA YA KUZINGATI MAMBO HAYA MUHIMU

Mara nyingi tumekuwa tukisikia baadhi ya kinadada wakilalamika kuwa wamepata ujauzito kwa bahati mbaya, hili ni jambo amablo hujitokeza sana lakini si nzuri kwani ujauzito mara zote huwa unahitaji mipango.

Kwa kawaida wakati wa kipindi cha ujauzito kuna mambo mengi huweza kutokea hususani mabadiliko ya mwili.

Hata hivyo, kuna baadhi ya mambo ya kuzingatiwa kabla ya kuamua kushika ujauzito 

Kwanza kabisa kuwa na mpango maalum wa siku au mwezi gani utakuwa tayari kushika ujauzito, ili uweze kujipanga zaidi kuanzia kisaikolojia lakini hata kifedha pia.

Jambo jingine muhimu ni kufanya uchunguzi wa afya yako, kwanza nilazima ufanye uchunguzi ili kutambua ikiwa unamagonjwa mbalimbali yakiwemo yale magonjwa yasiyoambukiza kama vile siko seli, kifafa, shinikizo la damu, saratani bila kusahau kupima maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Pia ni vyema kuhakikisha huna huna magonjwa katika viungo vya uzazi, mfano matatizo ya fangasi au U.T.I na mengine mengi yanayoambatana na hayo.

Aidha, kama unatarajia kushika ujauzito, pia ni vyema ukaachana na tabia ya kutumia vilevi na badala yake jenga utaratibu wa kunywa juisi za matunda mbalimbali kwa ajili ya kuupa mwili virutubisho muhimu, lakini pia kutumia zaidi mboga za majani mara kwa mara kadri uwezavyo.

Kitu kingine cha msingi wakati ukitarajia kushika ujauzito ni pamoja na kufanya mazoezi japo yale mepesi, hii itakusaidia kuandaa viungo vyako kuwa vizuri zaidi kupokea mtoto hususani nyonga na kukufanya kuepuka kukumbwa na matatizo wakati wa kujifungua. Zangatia mazoezi unaweza kufanya japo yale mepesi mepesi kidogo.
Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara ili kuimarisha nyonga na viungo vyako vingine na usipate matatizo wakati wa kujifungua. Pata ushauri wa daktari kipindi muafaka.

Kumbuka kwamba kuna baadhi ya sababu ambazo zitaweza kusababisha mwanamke kushindwa kushika ujauzito, sababu hizo ni pamoja na mirija ya uzazi kuziba, uvimbe kwenye kizazi pamoja na maambukizi ya sehemu za via vya uzazi kama vile fangasi na U.T.I, hivyo ikiwa unahitaji kushika ujauzito kirahisi ni vyema ukamali kabisa magonjwa  ya namna hiyo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment