Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 22 October 2015

USIKUBALI KUTESEKA NA TATIZO LA HARUFU MBAYA SEHEMU ZA SIRI, ZIPO HAPA NJIA ZA KUKABILIANA NA TATIZO HILO

Ishu ya kutokwa na harufu mbaya sehemu za siri au uchafu sehemu za siri ni moja ya tatizo ambalo limeonekana kuwasumbua wanawake wengi na baadhi yao kujikuta wakikosa amani kabisa hata wanapokuwa na wenzi wao au wanapojumuika na kundi la watu.

Mandai Herbalist Clinic kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo leo Oktoba 22, 2015 tumeona ni vyema tukawafahamisha mambo muhimu yanayoweza kuwa msaada kwa wanawake wenye tatizo hilo.

Yafuatayo ni mambo ya msingi ya kuzingatia ili kuepuka hali hiyo>>>

Kwanza mwanamke anapaswa kuzingatia kufanyia usafi sehemu zake za siri kwa kutumia maji safi na salama kila unapomaliza kujisaidia haja ndogo. Tambua kwamba huu ni utaratibu muhimu sana kwa wanawake ili kuepuka madhara ya kuingia katika tatizo hilo.

Kumbuka kwamba unapokuwa unajisaidia haja ndogo yako inapotoka lazima kutakuwa na mabaki kidogo yatabaki kwenye mashavu ya sehemu zako za siri. Hivyo hayo mabaki baada ya muda yatachanganyikana na jasho na kisha kutengeneza harufu mbaya ndio maana inaimizwa kujisafisha kila unapomaliza kujisaidia haja ndogo. 

Kitu kingine cha msingi ili kuepuka hali tatizo hili ni kuvaa nguo za ndani zenye asili ya pamba, hii ni kwa sababu pamba huwa na uwezo wa kupitisha hewa na sehemu za siri za mwanamke huhitaji hewa inayoingia na kutoka. Hata kama hewa inaingia kwa kiasi kidogo bado itasaidia kufanya sehemu hizo za siri kuwa katika hali nzuri na kushindwa kuingia kwenye tatizo hilo.

Acha kuvaa nguo zenye kubana sana muda wote, kwasababu nguo za kubana husababisha majasho sehemu za siri na hivyo kuchangia sehemu hizo kutoa harufu, lakini pia epuka kuvaa nguo ya ndani moja siku nzima bila kubadilisha, kutokana na maumbile ya mwanamke yalivyo, mwanamke anapaswa kubadili nguo ya ndani mara mbili au tatu kwa siku. 

Aidha, unapokuwa kwenye siku zako ni vyema kubadilisha pads mara kwa mara hii itakusaidia kuwa na amani na kuzuia bakteria kujikusanya na hivyo kuzuia kutoa harufu mbaya sehemu zako za siri.

Jambo jingine muhimu ni kuhakikisha unanyoa nywele zako za sehemu za siri mara kwa mara kwa sababu nywele hizo zinapokuwa ndefu hutengeneza maficho ya kila aina ya uchafu ikiwa ni pamoja na jasho pamoja na majimaji yanayokutoka ukeni na yale mabaki ya haja ndogo hali ambayo husababisha harufu pia.

Halikadharika ni vyema kuosha sehemu zako za siri kwa kutoka mbele kurudi nyuma, wakati uanajisafisha unapopeleka mkono nyuma unakuwa kama unazoa bakteria na uchafu kwenye uke, na huo ndio utakuwa mwanzo wa sehemu hiyo ya siri kuanza kutoa harufu mbaya.

Kama unasumbuliwa na tatizo hili au kutokwa na uchafu ukeni basi usipate shida kwani  unaweza kupata msaada zaidi wa kimatibabu kutoka kwa Tabibu Mandai mpigie sasa kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment