Friday, 9 October 2015

UTAFITI MWINGINE KUHUSU MADHARA YA SIGARA, VIFO HUENDA VIKAONGEZEKA IFIKAPO 2030


Si jambo geni kabisa kusikia wataalam wa afya wakizungumzia madhara yanayoweza kupatikana kutokana na matumizi ya sigara, lakini bado watu wameendelea kuvuta pasipo kujali afya zao

Sasa leo kuna utafiti mpya ambao unaeleza kuwa sigara ina uwezo wa kuua kijana mmoja kati ya vijana watatu nchini China.

Kwa mujibu wa utafiti huo umeeleza kuwa hali hiyo huenda ikatokea endapo hapatakuwa na hatua yoyote itakayofanyika kwa lengo la kuwafanya vijana kuacha kuvuta sigara.

Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la Lancet linalohusiana na masuala ya tiba, unasema kuwa China inakabiliwa na ongezeka kubwa la vifo vya mapema kwa kuwa theluthi mbili ya vijana nchini humo huanza kuvuta sigara wakiwa chini ya miaka ishirini na karibu ya nusu ya vijana hupoteza maisha kutokana na tabia zao.

Pamoja na hayo kwa mujibu wa utafiti huo umeeleza kuwa endapo hali hiyo ya sasa itaendelea, basi idadi ya watu wanaokufa kutokana na matumizi ya tumbaku kila mwaka nchini China itaongezeka, wengi wao wakiwa ni wanaume ambapo watafikia watu milioni mbili ifikapo mwaka 2030.

Wanasayansi walifanya tafiti mbili kwa nchi nzima ndani ya miaka kumi na tano ukiachilia mbali ufuatiliaji wa athari za kiafya kutokana na uvutaji sigara nchini China.

No comments:

Post a Comment