Friday, 2 October 2015

UWEZO MWINGINE WA MAJI YA DAFU KATIKA TIBA SIKU YA LEO

Mawe kwenye figo ni tatizo ambalo hutokea kutokana na upungufu wa vitamin fulani vinavyosababisha kuganda kwa kemikali za chumvi katika mkojo na kutengeneza vitu vigumu kama mawe ndani ya mkojo.

Dalili ya tatizo la mawe kwenye figo ni pamoja na kwenda haja ndogo mara kwa mara, kuhisi maumivu wakati wa kukojoa na kupata haja yenye mchanganyiko wa usaa na damu.

Dalili nyingine ni kuhisi maumivu ya mgongo, maumivu ya kibofu pamoja na homa ambazo huambatana na kutetemeka na homa.

Baadhi, ya vitu ambavyo husaidia kutatua tatizo hili ni kama hivi vifuatavyo:

Tikiti Maji
Kula tunda hili mara kwa ra husaidia sana kwa watu wenye tatizo hili.

Maji ya Dafu.
Kunywa maji ya dafu glasi mbili kila siku yaani asubuhi na jioni kwa muda wa mwezi mmoja.

Zabibu.
Jenga utaratibu wa kula zabibu mara kwa mara husaidia sana kuhusu tatizo hili, lakini ukiona hali bado ni vyema ukafika kwenye kituo cha karibu cha afya kwa uchunguzi zaidi.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment