Friday, 23 October 2015

VIAZI MVIRINGO HUONDOA TATIZO LA MICHIRIZI MWILINI, SOMA HAPA NAMNA YA KUVITUMIA

Tatizo la kutokwa na michirizi kwenye ngozi ni moja ya mambo ambayo yameonekana kuwakumba wanawake wengi na kwa kiasi kikubwa wengi wao huonekana kukwazika na hali hiyo.

Ukikutana na mtu mwenye tatizo hilo unaweza kujua huenda alibata jeraha na akabakiwa na mabaka au kovu, lakini siyo kovu na wala mtu hakupata ajari au kuumizwa na kitu chochote.

Kwa kawaida au mara nyingi alama hizi za michirizi humtokea mtu maeneo ambayo huwa na nyama nyingi au mafuta ya kutosha, Mfano kwenye mapaja, upande wa juu wa mikono, tumboni, kwenye makalio, lakini pia baadhi ya watu hutokea maeneo ya kifuani au kwenye matiti kwa wanawake.

Hata hivyo kwa kawaida michirizi hiyo huwa haileti maumivu ya aina yoyote, isipokuwa hubadili muonekano wa ngozi ya muhusika tu, kwani baadhi ya watu michirizi hiyo huweza kuwa ni mikubwa sana na kumkosesha amani mhusika.

Tatizo hili huchangiwa na kuongezeka kwa uzito kwa ghafla au wengine huweza kukumbwa na tatizo hili kutokana na aina ya ufanyaji wa mazoezi fulani fulani.
Viazi mviringo ndio ni suluhisho
Moja ya tiba asili ya tatizo hili ni pamoja na matumizi ya viazi mviringo.

kinachofanyika ni kupata vipande vidogo vidogo vya viazi hivyo kisha mhusika atasugua sehemu yenye tatizo na ataacha kwa muda usio pungua saa moja kisha ataosha kwa kutumia maji ya uvuguvugu, njia hii ukitumia kwa muda mrefu kutwa mara mbili kila siku husaidia sana kuondosha michirizi hiyo.

Pamoja na hayo ni vyema kuzingatia kunywa maji ya kutosha kila siku kwani maji hayo husaidia kuondoa sumu mbalimbali mwilini kupitia ngozi na hivyo hukuwezesha kuwa na ngozi yenye afya nzuri zaidi

Kwa maelezo au ushauri zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment