Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 12 October 2015

VIFAHAMU HIVI VIASHIRIA AMBAVYO HUMAANISHA MZUNGUKO WAKO WA DAMU MWILINI HAUPO VIZURI


Mzunguko mzuri wa damu husaidia sana binadamu kuwa na afya nzuri zaidi, hii ni kwa sababu damu inapozunguka ndipo hufanya kazi ya kusafirisha virutubisho mwilini pamoja na hewa ya oksijeni kila kona ya mwili.Hivyo pale inapotokea binadamu akawa na mzungumko ambao si mzuri ndani ya mwili huweza kuwa na madhara.

Mzunguko ambao si mzuri wa damu mwilini (poor blood circulation) huweza kusababishwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa kama kisukari, magonjwa ya moyo, unene kupita kiasi, lakini pia tatizo hili huwakuta kinamama wajawazito pia.

Ikiwa tatizo hili halitapata mfumbuzi wa haraka huweza kupelekea mhusika kupatwa na kiharusi 'stroke' pamoja na mshtuko wa moyo yaani 'heart attack' na mara nyingine huweza kupelekea kifo kwa mhusika.

Zifuatazo ni dalili zitakazokuonesha kwamba mzunguko wa damu yako mwilini haupo vizuri zipate hapa>>>>

Kuhisi ganzi mikononi na miguuni, unapoona unapatwa na ganzi mara kwa mara hasa sehemu za miguu na mikono jua kwamba si dalili zuri na huenda tayari mzunguko wa damu mwilini haupo sawa hivyo ni vyema kuonana na wataalam wa afya kwa ushauri zaidi.

Dalili nyingine ni kuhisi ubaridi mikononi na miguuni, kwa kawaida mzunguko mzuri wa damu mwilini husaida kuupa mwili joto, hivyo mzunguko unapokuwa si wakawaida basi hali hiyo husababisha mikono na miguu kuwa na ubaridi zaidi.

Mtu ambaye hana mzunguko mzuri wa damu mwilini  (poor blood circulation) mara zote yeye huisi uchovu hata kama hakuna kazi yoyote kubwa aliyofanya ya kumsababisha kuchoka, hivyo unapokutana na hali hiyo inakusa kufika kwenye kituo cha afya kwa ushauri zaidi.

Tatizo hili pia huchangia mhusika kutokuwa na kinga za mwili imara, hali hii hutokana na kutokuwepo kwa usafirishaji mzuri wa virutubisho mwilini na hivyo kuchangia kinga za mwili kushindwa kuwa imara zaidi

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment