Tuesday, 13 October 2015

VIFAHAMU VYAKULA AMBAVYO UNAWEZA KULA WAKATI WA BARIDI

Watu wengi huwa hawafahamu ni vyakula gani hufaa kuliwa kipindi cha wakati wa baridi hivyo leo hii nimekuwekea hapa baadhi ya vyakula hivyo.

Karanga ni miongoni mwa vyakula muhimu katika kipindi cha baridi, hii ni kutokana na uwezo wake wa kuongeza joto la mwili. Pia karanga ni chanzo kizuri cha vitamin E na B3, halii kadhalika karanga husaidia sana kwa afya ya moyo.

Ulaji wa maboga pia hufaa zaidi katika kipindi cha baridi, huku ikisaidia kuondoa baadhi ya sumu mwilini na kupunguza unene zaidi kwa wale wanene kupita kiasi.

Pia matumizi ya juisi ya maboga ni nzuri zaidi kutokana na kuwa na utajiri wa beta-carotene pamoja na vitamin E, huku ikisaidia pia kutoa kinga dhidi ya athma.

Viazi vitamu pia ni chakula kizuri sana chenye vitamin nyingi na kizuri sana wakati wa kipindi cha baridi na huongeza joto la ziada mwilini, hali kadhalika viazi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi yaani ‘fiber’ pamoja na vitamin A, C na madini ya ‘manganese’ na ‘copper’. Unaweza kula viazi hivyo mara baada ya kuchemsha.

Kabeji ni mojawapo ya mboga yenye umuhimu katika mlo, kutokana na kuwa na virutubisho vya kutosha, pia ni moja ya mboga yenye vitamin A na ndani yake ina madini ya lutein na zeaxanthin, ambazo zote ni muhimu kwa afya ya macho pia.

Kabichi ni nzuri pia inapotumika katika kipindi cha baridi ambapo inaweza kutengenezwa kama kachumbali.

Mboga za majani nazo zinapendekezwa kuliwa katika kipindi cha baridi, hususani 'spinachi' ambayo huwa na utajili wa virutubisho vya ‘antioxidants’ na madini chuma . Antioxidants ni chanzo kizuri cha nishati mwilini ambayo husaidia kupunguza hali ya ubaridi mwilini.

Kwa maelezo zaidi wasiliana  na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment