Thursday, 8 October 2015

VIFO VYA MAHUJAJI WA TANZANIA WALIOFARIKI MAKKA VYAONGEZEKA SASA WAFIKIA 11Septemba 24, 2015 taarifa kubwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari duniani ilikuwa ni kuhusu vifo vya mahujaji zaidi ya 700 wakiwemo na watanzania pia ambao waliopoteza maisha kutokana na tukio la kukanyagana lililotokea katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudia Arabia.

Ripoti mpya ni kwamba serikali imepokea majina matatu ya mahujaji wengine wa Tanzania, waliokufa kutokana na tukio lhilo hivyo kufanya idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha nchini humo kuongezeka na kufikia 11.

Hayo yalithibitishwa jana na Serikali kupitia taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari. Taarifa hiyo iliwataja watatu zaidi waliokufa kuwa ni Yusuf Ismail Yusuf kutoka kikundi cha Khidmat Islamiya, Rahma Salim Suweid kutoka kikundi cha Ahlu Daawa na Issa Amir Faki.

Taarifa hiyo ilisema mahujaji hao walitambuliwa baada ya kupitia taarifa zao za vidole zilizotolewa na Serikali ya Saudi Arabia, huku serikali ikisema vifo hivyo vinaendelea kuwa pigo kwa taifa na kwamba, vimepokelewa kwa masikitiko makubwa.

"Aidha, Ubalozi unaendelea kushughulikia taratibu za maziko kwa mahujaji ambao wamefariki dunia na miili yao kutambuliwa. Tunapenda kufafanua kuwa mali za marehemu ikiwemo mizigo waliyokuwa nayo wakati wa Hijah zitawasilishwa nyumbani Tanzania na vikundi walivyokuja navyo na kukabidhiwa kwa jamaa wa marehemu,” ilieleza taarifa ya wizara.

Mbali na hayo, taarifa hiyo iliainisha  ubalozi unaendelea kufuatilia orodha mpya ya taarifa za vidole, iliyotolewa na Serikali ya Saudi Arabia kwa ajili ya kuwabaini mahujaji wa Tanzania ambao hawajatambuliwa. Huku mpaka sasa zaidi ya mahujaji 30 wa Tanzania hawajulikani

No comments:

Post a Comment