Saturday, 10 October 2015

YAFAHAMU MAMBO MUHIMU YANAYOZINGATIWA NA WANAWAKE KABLA YA KUANZISHA MAHUSIANO MAPYA

Leo  ni weekend hivyo nimeona ni vyema pia tukabadili hali ya upepe humu ndani ya tovuti yetu ya www.dkmandai.com na nimeona tuzungumze kidogo kuhusu mahusiano.

Tunapozungumzia mahusiano huwa kuna mambo mengi zaidi katika sehemu hiyo, lakini leo hapa napenda kuzungumza kuhusumambo muhimu ya kuzingatia kabla kuingia kwenye mahusiano na hii itawahusu zaidi kina dada au wanawake kwa ujumla.

Kwa kawida katika mahusiano kila mtu huwa anakuwa na vigezo vyake kabla ya kuamua kuingia kwenye mahusiano na mtu fulani.

Ninavyo hapa baadhi ya vigezo ambavyo hutazamwa au huzingatiwa na wanawake kabla ya kukubali kuingia kwenye mahusiano mapya:-
Kinadada wengi hupenda kuwa na mwanaume msikivu, hii ni kwa sababu wanawake hupenda sana kusikilizwa na mara nyingi wanawake hupenda mwanaume wa aina hiyo bila kujali kama anaweza kutatua matatizo yake au laa! Matatizo huweza kuanza katika mahusiano kama hakuna mawasiliano ya karibu na usikivu na hapo ndipo shida huanza.

Pia wanawake wengi hupendelea wanaume wenye kujiheshimu kuanzia kauli zao, mavazi ni ngumu kidogo kukuta mwanamke anakubali kirahisi kuanzisha mahusiano na mwanaume mwenye maneno machafu au asiye na adabu kwani wengi huamini kama ameshindwa kuwaheshimu wengine basi ipo siku atakuja kuwavunjia heshima na wao pia.

Wanawake wanapenda sana kuthaminiwa katika mapenzi hata kama ni kwa vitu vidogo vidogo sana katika mapenzi, hivyo kina dada wengi hufurahi zaidi kuingia kwenye mahusiano na wanaume wenye kutambua uthamani wa mwanamke.

Kwa wale wanaume waongeaji sana basi ni vyema ikafahamika kuwa mara nyingi kinadada huwa hawapendi sana wanaume wa aina hiyo  au wanaume wa kulalamika lalamika mara kwa mara au kila siku hii ni moja ya sababu ambayo wanawake wengi pia huizingatia kabla ya kuanzisha mahusiano.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment