Tuesday, 6 October 2015

YAJUE HAYA MAAJABU YA SAMAKI KATIKA KUIMARISHA AFYA YAKO YA NGOZI

Habari za Jumanne hii mpendwa msomaji wetu wa www.dkmandai.com bila shaka umzima kabisa.

Naomba tutumie siku hii ya leo kufahamu namna ya kuimarisha afya ya ngozi zetu kwa kutumia vyakula.

Vyakula  ambavyo napenda kuzungumzia leo ni vya baharini, hivi ni miongoni mwa vyakula muhimu sana katika kuimarisha afya ya ngozi.

Vyakula hivi hufaa kwa afya ya ngozi kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha Zinc na Omega 3 ambazo ni muhimu sana kwa siha ya ngozi.

Faida za 'Omega 3' ni pamoja na kuondoa ukakamavu au hali ya ukavu wa ngozi pamoja na kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi.

Aidha, vyakula hivyo husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi, kwani damu inapozunguka vyema mwilini afya ya ngozi nayo huimarika. 

Madini ya Zinc ambayo hupatikana kwa ulaji wa samaki nayo husaidia kuondoa harara na chunusi katika ngozi kwasababu huyeyusha homoni ya 'testosterone'. Pia husaidia kuzalishwa seli au chembe hai za mwili na kuondoa chembe zilizokufa huku ikiifanya ngozi ing'ae na kuwa na mvuto zaidi

Kwa maelezo zaidi au ushauri tutafute kwa mawasiliano yafuatayo 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Kwa wale wa facebook tupate kupitia ukurasa wetu uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc.

No comments:

Post a Comment