Friday, 30 October 2015

YAJUE HAYA MADHARA YA KUCHANGIA NGUO NA TAULO


Leo ni Ijumaa ya Oktoba 30, 2015, ikiwa ni siku tulivu kabisa nikiamini Watanzania wengi tayari wameanza kurejea katika shughuli zao za kila siku baada ya pilika pilika zote za Uchaguzi Mkuu. Ambao ulipelekea mgombea wa Chama cha Mapinduzi Dk John Pombe Magufuli kutangazwa kuwa mshindi na rais mteule ambaye anasubiri kuapishwa hivi sasa.

Lakini huo ulikuwa ni mwanzo tu, lengo langu ni kuhitaji kukupa haya maelezo kuhusu hii tabia ya kushare mavazi au taulo za kujifutia maji mwilini.

Mara nyingi hii tabia ya kuchangia nguo ipo sana kwa kinadada na kina kaka ni kwa kiasi kidogo sana lakini kimsingi tabia hiyo inamadhara yake ikiwa ni pamoja na kusababisha maambukizi ya baadhi ya magonjwa.

Tabia ya kuchangia nguo za kuvaa au taulo za kujifutia maji baada ya kuoga huchangia kwa kiasi kikubwa kueneza vimelea vya magonjwa kama fangasi,  upele, kisonono, kaswende nk.

Magonjwa hayo huweza kuenea kwa urahisi kupitia njia hii ya kuchangia nguo na mavazi ya aina nyingine au matandiko hivyo ni vyema ukajali afya yako kwa kuepuka kuchangia nguo na taulo ili kujiweka katika mazingira salama zaidi.

Kama utakuwa tayari umepatwa na maambukizi unaweza kuonana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784  300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment