Friday, 9 October 2015

ZIFAHAMU HAPA DALILI ZA FIGO YAKO KUWA NA TATIZO

Figo ni miongoni mwa viungo muhimu katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu, miongoni mwa kazi za kiungo hicho ni pamoja na kuchuja uchafu uliomo kwenye damu.

Figo pia huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku zikinyonya madini na kemikali muhimu na kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje uchafu usiohitajika. 

Kazi nyingine za figo ni pamoja na kusaidia kutengeneza mada ya erythropoletin ambayo ni muhimu katika utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu, hupokea asilimia 25 ya damu na kila figo ina chembechembe hai ndogo milioni moja, ambapo pia husaidia kudhibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure).

Aidha kwa kawaida huwa kuna viashiria vya tatizo la figo miongoni mwa viashiria hivyo ni pamoja na kuongezeka kwa uchafu ndani ya mwili ambao husababisha kupungua kwa kiasi cha mkojo, kushindwa kupumua, kusikia kichefuchefu, kutapika na kuvimba kwa miguu. 

Dalili nyingine ni maji kujaa mwilini, asidi nyingi, matatizo katika moyo, kukosa hamu ya kula na kudhoofika mwili.

Hali hiyo husababisha udhaifu, kuhema kwa shida, uchovu na kuchanganyikiwa. Kushindikana kuondolewa kwa kemikali ya potassiamu katika mirija ya damu husababisha mapigo ya moyo na kifo cha ghafla.

Wakati mwingine dalili zinaweza zisijitokeze hata kama tatizo lipo. Dalili nyingine kwa wagonjwa ambao hawagunduliki mapema ni kuvimba macho wakati wa asubuhi na uvimbe kupungua baadaye.

Nyingine ni kuvimba miguu asubuhi na kupungukiwa damu mwilini ambazo huweza kujitokeza kama dalili za kwanza.

Kwa maelezo zaidi au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment