Thursday, 8 October 2015

ZIFAHAMU HIZI SABABU 6 ZA KIAFYA AMBAZO ZITAKUFANYA UANZE KUTUMIA BILINGANYA LEO


Habari za leo mdau wa www.dkmandai.com bila shaka umzima wa afya tele, ikiwa leo ni octoba 08, 2015 ni vyema tuendelee kufahamishana mambo muhimu kuhusu afya zetu.

Leo napenda tuzungumzie kuhusu bilinganya hii ni aina ya mboga ambayo baadhi yetu huwa tunaitumia katika maisha yetu ya kila siku licha ya kwamba inaonekana kama mboga ya watu wa hali ya chini, lakini inafaida zake pia kiafya.

Mboga hii ya bilinganya unapoipika husaidia sana kwa wale wenye shida ya vidonda vya tumbo na kumpatia mhusika usingizi mwanana, hivyo kwa wale wenye shida ya kukosa usingizi (insomnia) wanaweza kutumia bilinginya.

Aidha, bilinganya husaidia sana kuharakisha kupona kwa magonjwa na kuleta afya nzuri ya mwili, lakini pia bilinganya huweza kusaidia kutibu majipu pia mara baada ya kuliponda.

Juisi ya bilinganya pia husaidia sana kuondoa sumu mwilini ambayo hutoka kwa njia ya haja ndogo (mkojo) , lakini mizizi ya bilinganya pia inapochemshwa huwa ni tiba ya minyoo.

Kwaa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment