Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 23 October 2015

ZIFAHAMU SABABU ZA MIGUU NA MIKONO KUFA GANZI NA KUWAKA MOTO

Miili yetu binadamu kuna wakati huwa tunajikuta tunazongwa na magonjwa mbalimbali 

Leo nimeona tuangalie hili tatizo la kuhisi miguu kuwaka  moto na kufa ganzi kwa miguu na mikono.

Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili na hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.

Miongoni mwa dalili za tatizo hili ni pamoja na kuhisi ganzi, maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi, kuhisi kama kuna kitu cha ncha kali kinakuchoma miguuni au kwenye vidole, kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.

Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika ni pamoja na upungufu wa virutubisho mwilini, hususani vitamin B, B complex.

Sababu nyingine ni matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi, licha ya kwamba si wote huwasababishia hali hiyo.

Pia uzito mkubwa wa mwili, nayo ni sababu ya kupelekea kwa tatizo hili , lakini pia ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu huweza kuchangia tatizo hili .

Hata hivyo, bado tatizo hili huweza kuepukwa kwa kufanya mazoezi ya mwili ili kupunguza uzito, kuishi maisha yatakayokufanya uepukane na magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu pamoja na kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha na kuacha kutumia dawa kiholela bila kupata ushauri wa kitaalam.

Kwa maelezo zaidi au kama unasumbuliw na tatizo la miguu kuwaka moto, kuvimba, kufa ganzi au kujaa maji wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment