Thursday, 22 October 2015

ZIFAHAMU SABABU ZINAZOCHANGIA MIGUU KUVIMBA NA KUJAA MAJI


Si ajabu kusikia baadhi ya watu wakilalamika kuhusu tatizo la kuvimba miguu au kujaa maji na kuwa na muonekano kama vile uvimbe.

Kimsingi kuna sababu za uwepo wa tatizo hili ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo ambapo kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi zake vizuri, husababisha damu kushindwa kufika vizuri katika viungo vingine vya mwili ikiwemo miguuni. 

Magonjwa ya ini nayo ni moja ya sababu ya miguu kuvimba hii ni kwa sababu magonjwa hayo huchangia kupunguza uwezo wa utendaji kazi wa ini ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa vitu muhimu vinavyopatikana katika damu mfano protin (albumin).

Lakini pia tatizo hili la miguu kujaa maji huweza kujitokeza kwa sababu ya kuongezeka kwa mahitaji ya mwili, mfano kina mama wajawazito huweza kupatwa na tatizo hili kutokana na miili yao kuwa na ongezeko la mahitaji ya damu ili kuweza kuutoshereza mzunguko mzima hadi kufika kwa kiumbe/viumbe walioko tumboni.

Hizo ni baadhi tu ya sababu za tatizo hili la kuvimba kwa miguu kwa maelezo zaidi na msaada pia unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Maandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment